Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana.
Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya
ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa
kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika katika
uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Balozi wa Kenya Mhe.
Robinson Githae na Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Hazara
Chana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Balozi wa Kenya Mhe. Robinson Githae baada ya kuwasili b katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Kushoto ni Naibu.
Makamu wa Rais akimpongeza Rais Kenyatta kwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya kenya katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Mhe. Samia Suluhu Hassan amemwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Amina Mohamed mara baada ya kuwasili Nairobi Kenya kumwakilisha Rais Dkt John Joseph Magufuli katika sherehe za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta leo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...