Klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam inatarajia kutoa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo mkoani Pwani siku ya jumapili ya tarehe 19.2017.Kambi hiyo ya siku moja itatoa vipimo vya afya, ushauri, matibabu na huduma mbalimbali za meno, macho, malaria, usafi wa mwili, minyoo, masikio, pua na koo (ENT), pamoja na magonjwa ya ngozi na kwa mara ya kwanza itaendesha vipimo vya kansa ya shingo ya uzazi
Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa kambi ya matibabu Bwana Frédéric Morel amesema amefurahishwa na maandalizi ya mwaka huu kulinganisha na miaka iliyopita. “Tumefurahishwa na ushirikiano tunaopata kutoka kwa makampuni na watu binafsi katika kuhakikisha kambi hii inafanyika kwa mara nyingine tena.pili, tunatarajia idadi ya watu kuwa mara mbili kulinganisha na mwaka uliopita”.
Alisema, Morel. mbali na kambi ya Kerege, klabu yetu pia mwaka huu imetoa huduma ya matibabu ya bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Msasani A. Hivyo tunaomba wakazi wa Kerege na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.” Frédéric Morel.
Mbali na hilo, Mwakilishi kutoka benki ya Diamond Trust, Bwana Sylvester Bahati amesema ushirikiano na klub ya Rotary ya Oyster Bay katika miaka mitano iliyopita umekuwa ni ushrikiano mzuri wenye kubadili maisha ya watu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...