Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma katika harakati yake ya kuhakikisha wanajenga kituo cha Redio ya jamii katika Halmashauri hiyo imepanga kuanzisha Tamasha la muziki kwa lengo la kupata fedha kujenga kituo cha Redio.
Kamati ya uanzishwaji Redio katika Hamashauri hiyo imependekeza kuundwa kwa kamati ndogo itakayoratibu kuanzishwa kwa Tamasha la muziki kwa lengo la kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha Redio.
Aidha mwenyekiti wa kamati ya uanzishwaji Redio ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Bwana Gwakisa Mwasyeba ambaye ni Afisa mipango wa Halmashauri hiyo alipendekeza majina ya kamati hiyo kuwa ni James komba Afisa utamaduni wa wilaya hiyo , Afisa manunuzi Robert Mahili, Abbas Masawe katibu wa mikutano ya madiwani , na Afisa michezo John Ligoho na kuwataka kuanza mikakati ya kuanzishwa kwa Tamasha hilo la muziki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...