Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC), inaendelea kesho Alhamisi Novemba 9, 2017 kwa michezo saba ambako Dar City itacheza na Majimaji Rangers ya Lindi.
Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Bandari jijini Dar es Salaam huku Real Mojamoja ya Iringa ikiwa wenyeji wa African Wanderers kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa wakati Shupavu na Sabasaba zitachuana mjini Morogoro.
Mashujaa ilikwisha kupata mpinzani ambaye ni Buseresere ambaye kabla aliifunga Isoko katika hatua ya awali. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
The Mighty Elephant itacheza na Makanyagio kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Namungo na Villa Squad nazo zinacheza kesho kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara .



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...