Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita amezindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa Zahanati Wilayani Chato ili kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Wilayani humo.

Mhandisi Robert Gabriel amezidua kampeni hiyo kwa kushirikiana na wananchi kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa viwili pamoja na Ofisi katika shule ya msingi Ilyamchele ambayo inaongezeko la wanafunzi 2,212 kutoka 1,700. Darasa la pili linawanafunzi 407 ambao wanasoma kwa awamu mbili hivyo, kufanya shule hiyo kuwa na mahitaji ya vyumba vya madarasa 28.

Akizungumza na wananchi baada ya kuchimba msingi Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Serikali inataka watoto wa Ilyamchele wafanane na watoto wa maeneo mengine kwa kukaa katika vyumba vizuri vya kisasa vyenye miundombinu ya kutosha na walimu wa kutosha. Hivyo, ametoa wito kwa wananchi wote kushirikiana na viongozi wote katika utekelezaji wa miradi hii ili kumaliza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga ukuta katika kituo cha afya Mganza Halmashauri ya Wilaya Chato.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amendelea na ziara hadi kijiji cha Mganza ambapo ameshiriki katika ujenzi wa kituo cha afya Mganza ili kuona hali ya wananchi kupata huduma katika vijiji inaimalika kwa kujenga Zahanati na vituo vipya vya afya.

Miradi hii inatekelezwa na vikundi vya mafundi walioungana kwa kujitolea kufanya kazi hiyo pasipo kuwa na malipo isipokuwa kupatiwa chakula wanapokuwa katika eneo la kazi. Wananchi na wadau wanashiriki kwa kuleta maji, mchanga, sementi, kokoto na kushiriki katika ujenzi.

Mafanikio haya yanatokana na juhudi za Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa baada ya kuwasili mkoani Geita baada ya uteuzi wake aliamua kutoa semina kuhusu mikakati na njia za kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Tarafa, Maafisa elimu wa Wilaya na Makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya zote.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akichanganya mchanga na simenti kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mganza (Chato) alipofanya ziara ya kikazi ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...