Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, leo ameshiriki katika Matembezi ya Hisani ya Kilomita Nne na Nusu yenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Green Ground- Oysterbay mara baada ya matembezi hayo, Makamu wa Rais alisema takwimu za vifo vya kina mama zimeongezeka, hivyo wazo la kusaida kuongeza idadi ya wakunga ambao watasaidia kupunguza vifo hivyo ni zuri sana. 

Makamu wa Rais alisema “nimefarijika kusikia kuwa mwaka 2016 matembezi haya ya hisani yalikusanya wastani wa shilingi milioni 290 pesa ambayo iliwekwa katika fungu la kusomesha wauguzi wakunga wapya 75 katika mafunzo ya ngazi ya cheti” . Makamu wa Rais alionesha kufurahishwa na malengo yaliyowekwa kwa miaka miwili ijayo ya kukusanya kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kusomesha wakunga wauguzi 400 katika ngazi ya cheti na diploma kwa njia ya masafa. 

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa moja ya chanzo cha vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua ni ukosefu wa wataalam wa kuwahudumia. Takwimu za Tanzania zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya akina mama hawaendi kujifungua katika vituo vyetu vya kutolea huduma kutokana na kukosekana kwa wataalam wa kuwahudumia akina mama hao. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Ssuluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Afya Mh.Ummy Mwalimu, huku wakitembea mapema leo wakati akiongoza a matembezi ya hisani kwa ajili ya kusomesha Wauguzi Wakunga , matembezi hayo ya kilometa 4.5 yalianzia kwenye viwanja  vya Green Grounds, Oysterbay jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
 Matembezi yakiendelea.


 Picha ya pamoja na Washiriki wa Matembezi hayo ya Hisani .

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...