NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

ULE msemo wa kiswahili wa "mgeni njoo mwenyeji apone", unaweza kutumika kufatsiri neema ambayo taifa limepata kufuatia ziara ya siku mbili nchini ya Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, pichani juu.
Mhe. Mimica alianza ziara yake Novemba 2, kwa kutiliana saini makubaliano na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mjpango, ambapo EU imeahidi kutoa kiasi cha Euro milioni 50 ambazo zitatumika kupeleka umeme vijijini.
Serikali inapambana kuhakikisha vijiji elfu 12 (12,000) ambavyo bado havina umeme nchini vinapata huduma ya umeme ifikapo 2020.Kwa mujibub wa Afisa Habari wa EU hapa nchini Bi.Susanne Mbise, msaada huo wa Euro milioni 50 utasaidia kupeleka umeme kwenye vijiji 3,000.
Ziara ya Kamishna Mimica, ililenga kutembelea shughuli mbalimbali ambazo EU imekuwa ikifadhili,
Miongoni mwa maeneo ambayo Kamishna Mimica alitembelea ni pamoja na bandari ya Dar es Salaam, ambapo akiongea na uongozi wa bandari hiyo, Kamishna Mimica a,lieleza utayari wa EU katika kusaidia kub oresha bandari hiyo kwani ina msada mkubwa sio tu kwa Tanzania bali pia kwa nchi majirani.
Kamishna Mimica pia ametembelea kituo kinachosaidia vijana cha Nafasi Art Space kilichoko  Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo aliweza kusikiliza maoni yao na kujadiliana nao masuala mbalimbali yahusuyo changamoto za ajira na pia ukatili dhidi ya mtoto wa kike. "Kamishna Mimica amesema EU itatoa Euro  milioni 500 ili kusaidia kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto". amesema Bi. Mbise.
Kamishna huyo wa EU, alikutana na kujadiliana na makampuni makubwa ya kibinafsi ili kuona jinsi sekta binafsi inavyofanya shughuli zake hapa nchini na ziara hiyo ilimuwezesha pia kukutana na viongozi wa asasi za kiraia hapa nchini.
 Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, (kushoto), akiwa na balozi wa EU nchini, Mhe.Roeland van der Geer, wakati amkizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili nchini Novemba 3, 2017.(PICHA NA HABARI/K-VIS BLOG;Khalfan Said)
 Mhe. Mimica, akipokewa na Kaimu Mkurugezni Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, (TPA), Bw. Lazaro twange, alipotembelea bandari ya Dar es Salaam, Novemba 3, 2017. EU ni mdau mkubwa katika kjuisaidia TPA kuimarisha miundombinu yake.
 Mhe. Mimica akizun gumza na uongozi wa juu wa TPA.
 Mhe. Mimica akipeana mikono na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dotto James, baada ya kusaini makubaliano ambapo EU itatoa Euro milioni 50 kusaidia usambazaji umeme vijijini. Takriban vijiji 3,000 kote nchini vitafaidika na msaada huo. Serikali inapambana kuwafikishia umeme wana vijiji wa vijiji 12,000 a,mbavyo bado havijapata umeme na mpango huu umepangwa kukamilika 2020.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...