NA VICTOR MASANGU, PWANI

VIJIJI vipatavyo 54 katika mkoa wa Pwani ambavyo wananchi wake walikuwa katika hali ya sintofahamu kutokana na kukaa gizani kwa kipindi cha muda mrefu hatimaye wanatarajia kupata na kunufaika na nishati ya umeme wa uhakika ifikapo mwezi machi mwaka 2018 baada ya kukamilika kwa mradi wa kusambaza umeme vijiji (REA) awamu ya tatu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa wizara ya nishati Subira Mgalu baada ya kufanya ziara yake ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Bagamoyo pamoja na Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya kutembelea baadhi ya miradi ya REA ambayo inatekelezwa kwa awamu ya tatu pamoja na kujionea changamoto mbali mbali zinazowakabili.

Pia Magalu amesema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha inapeleka huduma ya uhakika kwa wananchi wake pamona na maeneo mengine yenye kutoa huduma za kijamii na kubainisha kuwa wanatarajia ifikapo mwaka 2021 vijiji vtote nchini view vimefikiwa na huduma ya nishati ya umeme.

Aidha Naibu Waziri huyo alipotembelea kituo cha uzalishaji wa umeme kilichopo maeneo ya Mlandizi aliliagiza Shirika la ugavi wa umeme Tanesco kuhakikisha wanajipanga vizuri ili kuweza kupunguza malalamiko ambayoyamekuwa yakitolewa na baadhi ya wananchi kuunguza vitu vyao majumbani kutokana na tatizo la kukatika katika umeme kila mara bila ya kutoa taarifa.
Naibu Waziri wa Wizara mpya ya nishati Subira Mgalu akizungumza na watendaji wa shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani pamoja na wakandarasi baada ya kukagua mradi wa REA awamu ya tatu uliopo maeneo ya sofu mlandizi Wilayani Kibaha mkoani Pwani alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kujionea mwenendo mzima wa ujenzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu wa kati kati akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu wa kushoto katika alipotembelea kituo cha usambazaji wa umeme kilichopo Mlandizi.
Naibu Waziri wa Wizara mpya ya nishati Subira Mgalu akipata ufafanuzi kutoka kwa wakandarasi wa mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu katika eneo la Msufini Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Naibu waziri mpya wa Nishati Subira Mgalu akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka kwa Meneja wa tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu wa kushoto mara baada ya kutembelea kituo cha umsambazaji wa umeme kilichopo Mlandizi ikiwa ni ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua miradi ya nsihati ya umeme 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...