Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani akiwa na kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Malindi Estate ambayo ipo kwenye nyumba ya mmoja wa wagombea wa Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata ya Mbweni. Picha na NEC.

Hussein Makame-NEC

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imejiridhisha kuwa uamuzi wa kuvihamisha vituo 21 vya kupigia kura katika Kata ya Mbweni, jimbo la Kawe katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, umezingatia Sheria na Kanuni za Uchaguzi.

NEC imetoa msimamo huo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi na vyama vya siasa wakilalamika kuwa Tume ya uchaguzi imehamisha vituo vinane (8) vya kupigia kura na kuvipeleka kwenye Kituo cha Polisi, hatua waliyoeleza kuwa ni kuwanyima haki wapiga kura katika kutimiza haki ya msingi.

Malalamiko mengine yaliyoifikia NEC ni kwamba Tume ilivihamisha vituo vingine 15 kutoka maeneo ya awali na kuvipeleka maeneo mengine jambo ambalo baadhi ya vyama havikukubaliana na uamuzi huo.

Kutokana na malalamiko hayo, jana Jumanne Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani akiambatana na watendaji wengine wa Tume, walitembelea maeneo hayo na kujiridhisha kuwa mabadiliiko ya vituo yaliyofanywa na msimamizi wa uchaguzi yamekidhi matakwa ya kisheria.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...