Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge amewataka watumishi wa Umma na Taasisi mbalimbali kwenye Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuwahudumia Wananchi kikamilifu na kwa uadilifu wakitambua kuwa sasa Mkoa wa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.
Aidha amesema yapo baadhi ya maeneo Mkoa bado haufanyi vizuri hususani katika sekta ya elimu ambapo hali ya ufaulu hairidhishi.
Akiwa wilayani Mpwapwa katika ziara yake ya kutembelea wilaya za Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kujitambulisha Dkt. Mahenge amesema eneo la Elimu ya Msingi na Sekondari hali ya ufaulu hairidhishi ambapo Mkoa umeshika nafasi ya 24 kati ya Mikoa 26 kwenye matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017, Wakati kwa upande wa Matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya Sekondari kidato cha nne mwaka 2016 Mkoa ulikuwa wa 19 kati ya Mikoa 26.
Amesema viongozi hao wanayodhamana kubwa kwa Wanadodoma kwenye masuala yote ya maendeleo kama vile Elimu, Afya, Kilimo, Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kutumia fursa ya kuwa jirani na Serikali katika kusukuma mbele masuala ya Maendeleo kwenye Mkoa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akikagua kitalu cha miche
ya Mikorosho ambayo itaanza kugaiwa bure kwa wananchi kwa lengo la
kuipanda na kukuza kilimo cha zao la korosho wilayani Mpwapwa
Sehemu
ya Kitalu cha Miche ya Mikorosho kilichopo eneo la Magereza Mpwapwa,
jumla ya tani sita (6) za mbegu bora za mikorosho zimeoteshwa kwa lengo
la kugawa bure miche ya mikorosho kwa wananchi kuipanda na kukuza kilimo
cha zao hilo Wilayani Mpwapwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge namna miti ya mikorosho
ilivyozaa korosho kwenye shamba darasa la Magereza Mpwapwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua maendeleo ya ujenzi wa
Kiwanda cha kukamua mbegu za alizeti na usindikaji mafuta ya alizeti
cha mjasiriamali Ndg. Sangito Akyoo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...