Serikali kupitia
Halmashauri za Wilaya katika mwaka 2016 imetoa jumla ya Hekta 271,882.86 za
ardhi kwa vijana nchi nzima ili kufanya shughuli
za uzalishaji mali na kujipatia ajira.
Hayo yameelezwa leo,
Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana na
Watu Wenye Ulemavu Anthony Mavunde
alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Mhe. Aida Khenan juu ya
mpango wa Serikali kwa vijana wanaomaliza shule za msingi, Sekondarii na Vyuo
kwa kuwazesha kujiajiri.
“Serikali imeendelea kuimarisha utekelezaji wa
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao unalenga kuwasaidia vijana wahitimu wa ngazi
mbalimbali za elimu kuweza kujiajiri kwa kuwapa mikopo ya masharti nafuu na
mafunzo ya ujasiriamali,” alisema Mavunde.
Aliendelea kwa
kusema, katika kipindi cha mwaka 2013/2014 hadi 2016/17, Serikali kupitia mfuko
wa Maendeleo ya vijana imetoa mikopo ya masharti nafuu ya Shilingi Bilioni 5.8
kwa vikundi vya vijana 6,076 vyenye wanachama 30,380 katika Halmashauri za
Wilaya 157 kupitia SACCOS za Vijana.
Aidha Mavunde
amesema, kupitia programu ya kukuza ujuzi wa
nchi Serikali imeanzisha utaratibu maalum wa kutambua ujuzi uliopatikana
kupitia mfumo usio rasmi na kuurasimisha kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa
wale walio tayari kuhitaji na kuwapa vyeti vinavyotambulika.
“Utaratibu huu
unawapafursa vijana wetu ya kuendelea na mfumo rasmi wa mafunzo na pia
kutambulika na waajiri au watoa kazi,” alifafanua Mavunde.Vilevile amesema,
Serikali imerahisisha utaratibu wa uundaji wa Makampuni kupitia BRELA hivyo
vijana wengi wanaomaliza vyuo kuweza kuanzisha Makampuni na biashara
zinazowezesha kuajiri vijana wengi.
Hata hivyo, Mavunde
amewataka vijana wanaomaliza shule za msingi na sekondari kujiunga katika
vikundi vya kuzalisha mali na kusajiliwa rasmi kupitia sheria ya usajili wa
NGO’s.Aidha mpaka sasa
jumla ya vikundi vya vijana vya uzalishaji mali 10, 200 vimesajiliwa.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...