Leo majira ya saa kumi jioni Mwanariadha Ismail Juma Gallet amepata ajali ya pikipiki kugongana uso kwa uso na Fusso na kufariki papo hapo.

Ajali hiyo ilitokea Kijijini kwao Gendi Wilaya ya Babati - Mkoa wa Manyara.

Mwezi uliopita Ismail alivunja rekodi ya taifa kwa kukimbia dakika 59 sekunde 30 katika mbio za Nusu Marathon ambazo ni 21 Kilometres.

Marehemu Ismail Juma alikuwa kati ya wanariadha ambao majina yao yameshawasilishwa ofisi za TOC tayari kwa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Madola (2018 Gold Coast Commonwealth Games).

Tunasubiri taratibu zingine kutoka kwa familia ya wafiwa. Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Murara Babati.

Habari hizi zimethibitishwa na;  

1) Mzazi wa Marehemu
2) Uongozi wa Riadha Manyara

Kwa niaba ya Chama cha Riadha Tanzania natoa pole kwa familia yake, tunakiri kupata pengo ambalo halitazibika.

Huu ni msiba wa taifa, alikuwa aende kuitetea Tanzania kwa kusaka medali na kupeperusha bendera ya taifa; lakini Mungu amemwita mapema.

RIP Champ....

Wilhelm F. Gidabuday,
Katibu Mkuu,
Chama cha Riadha Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...