Balozi
wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa hafla ya
uzinduzi wa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya
TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China
(China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya
Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. Halfa hiyo ilifanyika ijumaa
iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (kulia) na
Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla
Vumilia (kushoto). PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG.
Baadhi ya wageni ambao ni wanaumoja wa CAAT wakifuatilia kwa makini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo
ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akitoa pongezi kwa umoja wa wanafunzi
waliowahi kusoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -
CAAT) kwa kuweza kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia
ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao
umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni
Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi
wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Mhandisi Betram Kiswaga. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.
Katika salamu zake Jaji Mihayo aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi
kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii ili waweze kujifunza mengi
zaidi.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Mhandisi Betram Kiswaga akizungumza wakati wa hafla ya
kuzindua kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya
TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa
ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association
of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China
nchini Tanzania, Wang Ke.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...