Mamlaka ya mafunzo ya ufundi VETA leo imekabidhi vyeti vya kuhitimu masomo ya ufundi stadi kwa vijana 8 wa mkoa wa Dar es saalam baada ya  kuhitimu masomo yao ya ufundi wa umeme wa majumbani pamoja na ufundi wa simu mara baada ya kumaliza kusoma kupitia aplikesheni  ya VSOMO na kuhitimu katika viwango vya VETA.
 Akikabidhi vyeti hivyo Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es saalam , Bw. Habibu Bukko aliishukuru  Airtel kwa ushirikiano wake na VETA kupitia  Aplikesheni ya VSOMO ambapo imekuwa ikifaidisha wanafunzi walioko mbali na vyuo vya VETA kuweza kusoma VETA wakiwa popote, vilevile alipongeza vijana hao kwa kutumia simu zao za mkonononi vyema na kuhitimu masomo ya  ufundi
 Alisema jitihada hizi za Kufanikiwa kutoa Masomo ya Ufundi stadi kupitia Aplikesheni ya VSOMO zinaenda sambamba na mikakati iliyojiwekea VETA na  serikali  kwa ujumla katika kutanua wigo ili kutoa wa elimu ya Ufundi stadi hata kwa jamii ambayo bado haifikiwa na miundombinu ya vyuo vya VETA mahali walipo ili  nao kuwawezesha kushiriki maendeleo ya jamii.
“Hadi sasa tunao zaidi ya vijana takribani 54 waliohiti masomo yao kupitia VSOMO na kukabithiwa vyeti vyao. “nawapongeza kwa dhati vijana hawa kwa kuhitimu masomo yao leo. Pia tunao wanafunzi 25  wanasubiri kupangiwa masomo ya Vitendo ili  kuhitimu na kupata vyeti . Nitoe wito kwao kujiandaa vyema kuingia kwenye mafunzo ya viyendo laikini pia kwa watanzania hususani vijana kutumia fursa hii kujisomea masomo ya ufundi  kwa kupitia mfumo huu wa VSOMO wakiwa popote VETA itawahudumua” alisema  Bw. Bukko.
 Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam Bw. Habibu Bukko akikamkabidhi Cheti Mhitimu wa Mafunzo ya VSOMO kwa njia ya mtandao  Sunday Jabir ambayo ni ushirikiano baina ya VETA  na Kampuni ya Airtel Tanzaniam. Kushoto ni Meneja wa Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano.


 Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam Bw. Habibu Bukko akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO Jabir ambayo ni ushirikiano baina ya VETA  na Kampuni ya Airtel Tanzaniam. Kushoto ni Meneja wa Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano.
Meneja wa Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO Jabir ambayo ni ushirikiano baina ya VETA  na Kampuni ya Airtel Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam Bw. Habibu Bukko. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...