Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikao 12 ya Tanzania
inayoendelea na zeozi la kuwasajili wananchi kwa lengo la kuwapatia
Vitambulisho vya Taifa.
Kwa sasa zoezi hilo limeingia kwenye awamu ya pili ya Usajili
katika wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Bariadi, Meatu, Busega, Maswa na
Itilima huku mwitikio wa watu ukiwa mkubwa.
wanaoshiriki kwenye zoezi hilo ni wananchi wote wenye
umri wa miaka 18 na kuendelea, wageni na Wakimbizi.

Pichani ni Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwachukua alama za Kibaiolojia wananchi wa mkoa wa Simiyu Kijiji cha Mwakiboro wakati zoezi la Usajili likiendelea .

Zoezi la Usajili likiendelea katika Kijiji cha Kilulu wilayani Bariadi


Wananchi wa Kijiji cha Mwakiboro mkoani Simiyu wakisubiri kupatiwa huduma ya Uandikishwaji Vitambulisho vya Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...