Aliyekuwa katibu Mkuu wa Mkutano wa Beijing , Getrude Mongela akizungumza wakati wa mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Muasisi wa Mkutano wa Wanawake juu ya Amani na kutatua matatizo Barani Afrika, Dkt. Basirat Nahibi akizungumza juu ya suala la wanawake wa bara la Afrika kukutana kujadili na kuandaa upatanishi juu ya mgogoro wa kisiasa unaondelea nchini Kenya.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Mwanahabari Mwanamke mkongwe nchini Radhia Mwawanga akichangia hoja katika mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam jana
Mhariri wa jarida la mkutano wa Wajibu wa Mwanamke katika masuala ya Amani na kutatua Matatizo Barani afrika, Fatma Othman Moma akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...