Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika kwa Wananchama wa Chama cha Mapinduzi kutowapa nafasi za Uongozi wanachama wenye tabia ya kuhama Jimbo moja na kuhamia Jimbo jengine.

Alisema Wanachama hao hufikia uamuzi wa kuyakimbia Majimbo yao ya zamani na kutaka kuhamia majimbo mapya baada ya kujibaini kutowatumikia vyema Wanachama na Wananchi wao katika kipindi walichoomba ridhaa ya kuwawakilisha katika nafasi za Ubunge na Uwakilishi kwenye vipindi vya awali.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Magharibi wa kuwachagua Viongozi watakaouongoza Mkoa huo kwa kusaidiana na viongozi wengine katika kipindi cha Miaka Mitano ijayo 2017 – 2022 ambao ulifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema uzoefu umebainisha wazi kwamba Wawakilishi na Wabunge wanaoendelea na majukumu yao ndani ya Majimbo yao hukumbwa na matatizo ukiwemo ushawishi, fitna na majungu yanayobuniwa na wale wanaotaka nafasi hizo jambo ambalo huchangia kukosekana kwa uwajibikaji.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa Magharibi alipofika kuufungua Mkutano wao wa Uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni.
Balozi Seif akiufunguza Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mkoa wa Magharibi wa kuwachaguwa Viongozi wao wa kuwaongoza katika kipindi cha miaka Mitano ijayo kuanzia 2017 – 2022.
Baadhi ya Wajumbe wa Makutano Mkuu wa CCM Mkoa Magharibi wakiwa katika mchakato wa kuwachagua Viongozi wa Kuuongoza Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Baadhi ya Wajumbe wa Makutano Mkuu wa CCM Mkoa Magharibi wakiwa katika mchakato wa kuwachagua Viongozi wa Kuuongoza Mkoa huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mwenyekiti WA CCM Mkoa Magharibi aliyemaliza Muda wake Nd. Yussuf Mohad Yussuf akitoa nasaha na kuwashukuru wanachama na Viongozi wa Mkoa huo alioshirikiana nao na kumuwezesha kutekeleza majukumu yake katika muda wake wa utumishi wa Miaka 15 kwenye nafasi hiyo. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...