Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema wizara yake haitasita
kumchukulia hatua mkandarasi yeyote endapo atabainika kuwa chanzo cha
kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini.
Aweso alizungumza hayo wakati akiwa ziarani katika mkoa wa Songwe, akikagua
miradi ya maji katika Wilaya ya Momba.
Akiwa kwenye mradi wa Sogea uliopo katika mji mdogo wa Tunduma, amesema
endapo mkandarasi wa Kampuni ya Best One aliyepewa kazi ya kujenga mradi huo
atashindwa kukamilisha kwa wakati, hawatasita kumchukulia hatua mara moja.
‘‘Serikali inataka mradi huu wa Sogea na miradi mingine yote ya maji nchini ikamilike
kwa wakati na wananchi waanze kufaidi matunda ya Serikali yao, ndio maana nipo
hapa kufuatilia hilo na wakandarasi waliopewa kazi wahakikishe wanafanya kazi usiku
na mchana ili kufanikisha hilo,’’ alisema Naibu Waziri Aweso.
Wakati huo Aweso ameagiza ameagiza Sh. bilioni 1 zilizotolewa na Rais John Magufuli
kwa ajili ya ujenzi mradi wa maji Sogea zitumike kwa uadilifu na kukamilisha mradi huo
ili kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa Sogea na maeneo ya jirani.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Iranda ameiagiza Idara ya Maji wilayani humo,
kutowapa tenda wakandarasi waasio na sifa ambao wanatuhumiwa kukwamisha juhudi
za Serikali katika kukabiliana na tatizo la maji, na atakayefanya hivyo atakuwa
amevunja sheria na atachukuliwa hatua.
Hii inatokana na taarifa kuwa baadhi ya miradi ya maji wilayani Momba kushindwa
kukamilika kwa wakati kutokana na uwezo mdogo wa kitaalamu kwa baadhi ya
wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisaini kitabu cha wageni
juu ya tenki la maji la mradi wa Sogea uliopo Wilaya ya Momba, mkoani Songwe.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akihutubia wakazi wa
Tunduma katika mkutano wa hadhara katika ziara yake katika Wilaya ya Momba,
mkoani Songwe.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akishiriki kuchimba sehemu
itakayowekwa miundombinu ya mradi wa maji katika Wilaya ya Momba, mkoani
Songwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...