Benki ya TPB Desemba 21, 2017 imechezesha droo ya pili ya Western Union na kupata washindi 7 kutoka matawi mbalimbali . Washindi 5 walipata simu za mkononi na 2 walipata kompyuta mpakato.
Majina hayo yalitajwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benk hiyo Bw. Mshamma Mshamma na kusimamiwa na Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.
Washindi waliojishindia simu za mkononi aina ya Samsung J5 ni Bi. Elizabeth Lugendo kutoka Dar es Salaam, Bw.Frank Tetea kutoka Korogwe Tanga, Bw, Jafari Msaki kutoka Arusha, Bi. Rose Maluka kutoka Dodoma na B. Anna Kasoga kutoka Ifakara -Morogoro.
Washindi wawili waliojishindia kompyuta mpakato ni Bw. Justine Muyanza kutoka Mwanza na Bw. Abdul Hurey kutoka Arusha.
Moja ya mfanyakazi wa benki hiyo akichanganya kuponi za droo ya pili Western Union wakati wa kumtafuta mshindi wa droo hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana.
Meneja wa huduma ya Western Union kutoka Benki ya TPB. Editha Lunyungu kushoto akihakiki majina ya washindi kwenye kopyuta mpakato wakati wa kumtafuta mshindi wa droo ya pili Western Union wakati wa kumtafuta mshindi wa droo hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana.
Kaimu ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Benki ya TPB, Bw. Mshamma Mshamma (kushoto) akisoma jina la mshindi katika droo ya pili ya Western union. kulia anae shuhudia ni mwakilishi kutoka Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.
Picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...