Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi ameumaliza mgogoro wa ardhi wa muda mrefu kati ya wakazi wa Mtaa wa Mtambani Vingunguti na mwekezaji wa kampuni ya PMM jijini Dar es salaam. 

Mwekezaji huyo wa Kampuni ya PMM inayojihusisha na uhifadhi wa mizigo alitaka kuchukua eneo la hekari 228 lenye nyumba 4,000 na wakazi 70,000 wa Mtaa wa Mtambani Vingunguti. Waziri Lukuvi amesema Serikali haitambui uwekezaji uliokuwa ufanyike na kwamba, mwekezaji hakufuata utaratibu uliyowekwa na Serikali, hivyo kusababisha mgogoro huo kuwa mkubwa. 

Kwa mujibu wa wananchi wa eneo hilo tangu mwaka 2012 mwekezaji huyo aliwazuia kufanya shughuli zozote za uendelezaji kwa kile alichodai ameshafanya tathmini na anaisubiri Wizara ya Ardhi ambayo inamchelewesha, jambo ambalo Waziri Lukuvi amekanusha. 

Mwekezaji huyo ametakiwa kurejesha nyaraka alizozichukua kwa wananchi hao kinyume na utaratibu na ametakiwa kuwalipa fidia wananchi kwakuwa aliwazuia wakazi hao kufanya shughuli zozote za uendelezaji kwa kile alichodai ameshafanya tathmini. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kinachoendelea na malipo hayajafanyika. 

Waziri lukuvi aliwaambia wananchi hao kuwa kuanzia leo haya maeneo ni mali ya wananchi kama anataka kununua aanze upya kufuata utaratibu uliowekwa, na haiwezekani mtu anakuja kuwanunua watu 70,000 kienyeji. 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Vingunguti wakati alipoamua kusitisha zoezi la uuzwaji wa nyumba za Buguruni mpaka Vingunguti kwa Muwekezaji wa kampuni ya PMM ambaye amekuwa na mchakato wa kununua nyumba hizo kinyume cha utaratibu wa Serikali katika kufanya ununuzi huo na Tathmini
Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa akizungumza na Wananchi wa Vingunguti wakati wa kusikiliza Kero za Wananchi juu ya mradi wa PMM 
Mkuu wa Wilaya ya  Ilala Sophia Mjema akizungumza wakati wa Mkutano wa Waziri Lukuvi na Wananchi wa Vingunguti juu ya mradi wa PMM
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi Akipata
Maelezo ya mradi wa ununuzi wa nyumba za Vingunguti

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani juu ya Mradi wa PMM Ulivyowazungusha wananchi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, akishangiliwa na Wananchi wa Vingunguti mara kutangaza kuwa mradi wa PMM Autambuliwa na Serikali
Wananchi waliohudhuria Mkutano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  juu ya mradi wa PMM.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...