Na Mathias Canal, Njombe
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amesifu
juhudi za uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa utendaji
kazi kwa ubunifu kwa kuanzisha Mradi Wa kuongeza uwezo Wa kuhifadhi Mazao.
Mradi huo utahusisha ujenzi Wa Vihenge vya kisasa, Mghala ya
kisasa pamoja na ukarabati Wa Ofisi ambapo baada ya mradi huo kukamilika wakala
utakuwa umeongeza uwezo Wa kuhifadhi Shehena ya mahindi ya uzito Wa zaidi ya
Tani 250,000 ambapo Vihenge vya kisasa ni 190,000 MT na Maghala 60,000 MT.
Mradi huo unataraji kutekelezwa na kampuni mbili za kandarasi
kutoka serikali ya Poland (Feerum na Unia Arab) kwa usimamizi Wa Wakala Wa
Majengo Tanzania (TBA) ambapo unataraji kugharimu zaidi ya Bilioni 150 za
Kitanzania.
Tayari maandalizi ya awali yameshakamilika ikiwemo Utiwaji saini
mikataba, Uchunguzi Wa udongo, Tathmini ya athari ya Mazingira, Pamoja na
kutembelea eneo la mpango kazi.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo desemba 1, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakulima wa Mji wa Makambako, Mkoani Njombe katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Desemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo desemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba ya namna ya ununuzi na uhifadhi wa mahindi kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Desemba 1, 2017.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...