Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amekagua ujenzi wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu-NBS mjini Dodoma na kutoa wito kwa wakandarasi
wanaojenga miundombinu mbalimbali yakiwemo majengo kutumia malighafi
zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea
ukuaji wa uchumi.
Amesema
hayo baada ya kushuhudia mkandarasi anayejenga jengo hilo Hainan
International Ltd ya China, akitumia vifaa mbalimbali vya ujenzi
vinavyopatikana hapa nchini zikiwemo mbao na vifaa vya umeme, hatua
ambayo amesema inachangia kuwaongezea kipato wananchi.
Akizungumzia
ujenzi huo, Dkt. Mpango amesema jengo hilo litatumika ni muhimu kwa
maendeleo ya Taifa kwakuwa litatumika kuchakata takwimu mbalimbali
zitakazotumika katika kutunga sera na mipango mbalimbali ya kuendeleza
nchi.
“Huwezi
kupanga mipango yoyote bila kuwa na takwimu nzuri na bora, hapa ndipo
vile “vichwa” vyetu vya takwimu nchini vitachakata takwimu hizo ndipo
zitumike katika kutunga sera bora kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu”
Alisistiza Dkt. Mpango
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), akitoa maelekezo wakati alipokagua ujenzi wa Jengo la ghorofa 5 la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa na kushoto kwake ni Mhandisi Mshauri Bw. Abdulkarim Msuya.
Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya (kulia) akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa, (wa tano kulia) mjini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...