Na Said Mwinshehe, Globu ya Jamiii

MTOTO wa kwanza wa mwanamuziki Nguza Vicking, Nguza Mbangu amesema Mungu ameonyesha ukuu wake na kuifanya familia yao iliyokuwa kwenye kilio cha muda mrefu sasa kuwa kwenye shangwe. 

 Nguza ambaye kwa sasa anajulikana kwa jina la Nabii Michael amesema hayo leo jijini Dar es Salaam nje ya gereza la Ukonga ambalo baba yake mzee Nguza alikuwa akitumikia kifungo cha maisha kabla ya Rais Dk. John Magufuli kumuachia kwa msamaha wa Rais baada ya kutangaza kusamehe wafunga 8157 akiwamo mwanamuziki huyo na mwanaye Papii Kocha.

Nguza Mbangu amesema kilichotokea ni mapenzi ya Mungu kwa kuonesha ukuu wake huku akimshukuru Rais kwa kutoa msamaha huo, amesema familia itatoa tamko rasmi baada ya Rais kumtoa mzee wao kifungoni.  

 "Tutatoa tamko la familia kwa kilichotokea ila niseme tunamshukuru Mungu kwa kuonesha ukuu wake. Pia tunamshukuru Rais kwa uamuzi wake" amesema. 

Naye mwanamuziki maarufu King Kikii aliyekuwa nje ya gereza hilo baada ya kupata taarifa za kuachiwa Nguza Viking amesema kuwa kilio cha muda mrefu ambacho watanzania wamelia tangu Nguza Viking awe jela hatimaye imekuwa shangwe. Amesema  baada ya tamko hilo Nguza Viking amepigwa butwaa kwani haamin kama yupo huru lakini furaha imechukua nafasi yake.

Wakati huohuo mtoto wa kike wa Nguza Viking, Monica amesema anamshukuru Rais Mguful kwa kumtoa jela baba yake na kuongeza sasa furaha imerejea nyumbani. 

Nje ya gereza la Ukonga mashabiki wa mwanamuziki huyo wamejitokeza kwa wingi ili kumuona baada ya kuwa huru. Mara kadhaa baadhi ya askari magereza walizuia watu kusimama nje ya gereza hilo lakini watu waliamua kupiga kambi kuanzia saa saba mchana hadi jioni hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...