Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari M. Sururu amewataka Askari na Maafisa wa Jeshi la Uhamiaji kufanyakazi kwa Uweledi na kujituma ili kuweza kutekeleza vyema majukumu yao ya msingi ya kusimamia na kudhibiti Uingiaji, Ukaaji na Utokaji wa Watu Nchini. “Ili kuimarisha utendaji wetu ni vyema kuacha kufanya kazi kwa mazoea na muda wote, tutoe huduma za Uhamiaji bila ya Upendeleo, Unyanyasaji au Ucheleshwaji usio wa lazima. Tumieni lugha nzuri, zingatieni kwa vitendo dhana ya kumjali Mteja na Epukeni vitendo vya Rushwa wakati mkitoa huduma mbali mbali za Uhamiaji kwani Rushwa ni Adui nambari moja wa Haki” alisema Kamishna Sururu.
Kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu ndio mhimili mkuu wa mafanikio ya Taasisi yoyote ile ikiwemo ya Uhamiaji. Maafisa na Askari wa Uhamiaji wanapaswa kuheshimu na kutii Kanuni zote za kijeshi, “Idara yetu imeingia rasmi kwenye mfumo wa Kijeshi nasi hatuna budi kufanyakazi kwa Kasi, Ari na Mori kuhakikisha kwamba jukumu la Ulinzi na Usalama wa Mipaka ya Nchi yetu linatekelezwa ipasavyo” alisema hayo wakati akizungumza na Askari na Maafisa wa Uhamiaji waliopo Mkoa wa Kaskazini Pemba, akihitimisha ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba iliyoanza tarehe 18 – 21 Disemba, 2017. 
Aidha katika ziara hiyo, Kamishna Sururu alipata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali yenye changamoto za uwepo vipenyo na Bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa maeneo hayo, kwa shughuli mbali mbali zikiwemo za uvuvi na biashara, baina ya visiwa vya Pemba na Mombasa, Kenya. Kisiwa cha Pemba kinasemekana kuwa na Bandari bubu zaidi ya mia tatu (300) ambapo inaelezwa kuwa ni kimbilio kwa baadhi ya Raia wa Kenya na Raia wa Somalia ndani ya visiwa vidogo vidogo vilivyomo ndani ya Wilaya za Micheweni, Wete na Mkoani, Pemba. 

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akipokea salamu kutoka kwa Askari wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwasili Ofisi hapo kwa ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 - 21 Disemba, 2017. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Achacha.

Kamishna Sururu aliwasisistiza Askari wa Uhamiaji kuongeza Doria na Misako ili kuwabaini wale wote wanaojipenyeza na kuishi nchini kinyume cha Sheria za Uhamiaji nchini. “Pamoja na changamoto zilizopo kutokana na Jiografia ya Visiwa vya Unguja na Pemba, hatuna budi kusimamia vyema jukumu la Udhibiti wa Ungiaji na Utokaji wa Watu” “Kama mnavyoelewa jitihada mbali mbali zinazochukuliwa na serikali zetu zote mbili katika kuboresha utendajikazi wetu, Idara inatarajia kupata vitendeakazi pamoja na vyombo vya usafiri yakiwemo Magari na Pikipiki, ambavyo vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma zetu kwa Jamii” alifafanua Kamishna Sururu.

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Said M. Samaki akichangia hoja katika kikao cha pamoja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar na Wafanyakazi wote wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...