Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii.

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) imetaja majina sita kati ya wanane ya wajumbe walioteuliwa  katika Kamati ya kuchunguza na kufuatilia mali za chama.

Hatua hiyo imekuja kutokana na maagizo ya Mwenyekiti wa Umoja huo Kheir James kutaka kuhakikiwa kwa mali zote za umoja huo.

Akizungumza leo katika Makao Makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa umoja huo Shaka Hamdu Shaka ametaja majina ya wajumbe wa kamati hiyo ambayo itaongozwa na Mwenyekiti Maria Chaurembo.

Wengine ni Peter Kasera, Zelote Saitoti, Rose Manumbu, Sofia Kizigo na Elly Ngowi."Jukumu la kamati hiyo ni kufuatilia mali zote za umoja wetu, namna ambavyo zinatumika na mlolongo wa matumizi yake.

" Itaanza kazi haraka na wajumbe wengine wawili wa kamati hii wataungana na wenzao kufanikisha majukumu waliyopewa. Itakapomaliza kazi tutakuja kwenu kuelezea ambacho tumekibaini na nini cha kufanya,"amesema Shaka.

Amesema Mwenyekiti wao baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo moja ya majukumu ambayo ameamua kuanza nayo ni kufuatilia mali za chama na jukumu langu ni kuhakisha maagizo ya mwenyekiti wetu yanafanyiwa kazi tena kwa uhakika,"amesema Shaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...