Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Maelezo ya awali (PH) dhidi ya Afisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi anayekabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo la kukutwa akimiliki magari 19, mali isiyolingana na kipato chake yatasomwa Januari 11, 2018.
Jenipher alipaswa kusomewa maelezo hayo ya awali leo lakini Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter alieleza mahakama ni hapo kuwa bado hawajamaliza kuiandaa. Na kuomba ipangwe tarehe nyingine
Hakimu Huruma Shaidi anayesikiliza kesi hiyo ameahirisha hadi Januari 11, mwakani itaanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya Machi 21,2016 na Juni 30,2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19.
Nagari hayo ni Toyota RAV4, Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Viz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota Wish na Toyota Mark X.
Mengine ni Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry yote yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 Mali ambayo hailingani na kipato chake halali.
Pia anadaiwa kikutwa akiishi maisha ya kifahari yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...