Na Bashir Yakub.
Yafaa kujua utaratibu unaotakiwa kufuatwa kabla ya kufutiwa hati miliki ya
ardhi (nyumba/kiwanja). Unapojua utaratibu huu ndipo unapojua kama
ulionewa au hapana. Na kuonewa ni pamoja na kukiuka utaratibu. Na kukiuka
taratibu yoyote ya kisheria kunabatilisha mchakato wa kufutwa kwa hati yako
na kutakiwa kurudishiwa eneo lako au fidia.
Makala yaliyopita tulieleza mambo ambayo ukifanya unahesabika kukiuka
masharti ya umiliki wa ardhi na ni hapo unapoweza kufutiwa umiliki. Leo
tuangalie utaratibu wa kufuta umiliki ikiwa imethibitika kuwa tayari umekiuka
masharti hayo. Sheria namba 4 ya 1999 , Sheria Ya ardhi imeeleza utaratibu
wa kufuta umiliki wa ardhi.
UTARATIBU.
1.Ni lazima uwe umekiuka masharti au moja ya masharti uliyopewa wakati
unakabidhiwa ardhi/hati kwa mujibu wa kifungu cha 48 ( 1) cha Sheria ya
ardhi. Usikubali kufutiwa umiliki ikiwa hujakiuka sharti/masharti ya umiliki
uliyopewa, labda iwe vinginevyo.
2. Baada ya kuwa umekiuka masharti yafaa upewe taarifa maalum( notice)
kwa mujibu wa kifungu 48(2). Ni taarifa inayoeleza masharti ya umiliki
uliyokiuka na onyo la kufutiwa umiliki. Taarifa hiyo ni ya siku 90(miezi
mitatu). Taarifa hiyo utapewa wewe mmiliki na kila mwenye maslahi katika
ardhi hiyo mf, mpangaji, mrehani nk. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...