Na Yasini Silayo

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limewahakikishia Umeme wa uhakika wakazi wa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutokana na uboreshwaji mkubwa wa huduma za Uzalishaji, Usafirishaji na Usambazaji Umeme zinazoendelea katika Mikoa hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi alipofanya Ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara akiambatana na wajumbe wengine wa bodi pamoja na viongozi waandamizi wa TANESCO Makao Makuu na Kanda ya Kusini.

Akiongea na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoani Lindi, Dkt. Kyaruzi amesema kuwa tayari TANESCO imefanya matengenezo makubwa katika mitambo ya kuzalisha umeme wa Gesi wa Megawati 18. Mtambo huo unahudumia Mikoa ya Mtwara pamoja na Baadhi ya maeneo ya Lindi kupitia laini mpya ya 132kV Mtwara-Mahumbika iliyokamilika tangu mwezi Julai mwaka huu ikijengwa na mafundi wazawa kutoka ndani ya TANESCO kupitia kampuni Tanzu yake iitwayo ETDCO.

"Mbali na hali ya umeme kuimarika hivi sasa kutokana na matengenezo ya mitambo ya Mtwara, Shirika hivi sasa linaendelea na maandalizi ya ujenzi wa miradi miwili mikubwa ya Uzalishaji Umeme wa jumla ya megawati 540 Katika Mikoa hii pamoja na kuunga mikoa ya Kusini katika Umeme wa Grid ya Taifa kwa Laini kubwa ya Msongo wa Kilovolt 400. 
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt. Alexender Kyaruzi (katikati) na wajjumbe wa bodi ya Shirika hilo, wakipatiwa maelezo walipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika mkoani Lindi
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dkt. Alexender Kyaruzi akiongea na wananchi wa Mtama Mkoani Lindi wakati wa ziara ya Bodi ya wakurugenzi wa TANESCO Katika mikoa ya Lindi na Mtwara


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...