Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imezindua mradi wa Mradi wa Mtoto Mwerevu unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la IMA WORLDHEALTH, Pamoja na Chuo cha Cornel.
Lengo kuu la mradi huo ni kupunguza udumavu kwa asilimia 7 kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ambao unatekelezwa katika halmashauri 36 zilizo ndani ya mikoa mitano ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma.Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo amefungua kikao cha uhamasishaji mbinu za kupambana na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano kwa madiwani na watendaji kata.
Imeelezwa mradi huo utasaidia kuimarisha mikoa na halmashauri zake kwa kuzijengea uwezo wa watendaji wake wa sekta zote zinazohusika na masuala ya lishe kuhusu kupanga na kufanya ufuatiliaji wa shughuli hizo katika jamii.Pia utachangia fedha za utekelezaji kwenye bajeti na mipango ya mkoa na halmashauri 36 kwa njia ya ruzuku ya uwajibikaji na kuhakikisha fedha zitakazotolewa hazitaifanya mamlaka hizo za Serikali zisitenge fedha kwa ajili ya masuala ya lishe.
Hivyo badala yake utahamasisha ongezeko la bajeti ya shughuli za lishe kupanda katika kipindi chote cha mradi huo unapoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao cha uhamasishaji mbinu za kupambana na udunavu kwa watoto chini ya miaka mitano kwa madiwani na watendaji kata. Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti halmashauri hiyo, Mhe. Edward Shigela, Mwenyekiti wa halmashauri, Mhe. Boniphace Butondo na Afisa Lishe Wilaya, Avelina France.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Boniphace Butondo akifungua kikao hicho.
Washiriki wa kikao hicho wakiwemo madiwani na watendaji kata wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...