Na Obligado-Mtwara.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamtafuta Zuhura Ismail Mkazi wa Halmashauri ya Nanyamba Mkoani Mtwara kwa Kosa la Kumuua Aliyekuwa Mume wake kwa Kuchoma nyumba waliyokuwa wakiishii kwa kutumia mafuta ya Petrol kutokana na Wivu wa kimapenzi.

Zuhura ambaye anatafutwa na jeshi la Polisi,Majira ya Usiku alifika Nyumbani kwa mume wake huyo ambaye walikuwa wametengana na Kuhisi kuwa Ndani ya nyumba Mumewe alikuwa amelala na mwanamke Mwingine Hivyo Kuchoma Nyumba Moto na Kutokomea Kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amewaomba wananchii wanamfahamu kutoa taarifa popote watakapomuoa Mwanamke Huyo Zuhura Ismail.

Aidha kamanda Mkondya ameongeza kuwa Watu 12 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za Wizi wa pikipiki pamoja na Kuvunja nyumba za watu na kuiba Vifaa mbalimbali vya majumbani.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Limewataka wananchi waliotoa taarifa za kuibiwa wafike kituo cha Polisi kwa ajili ya Kutambua na kuchukua mali zao.
Pichani.Kamanda Wa Police Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya akiwaonesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) Samani za Ndani Zilizokamatwa baada ya Kufanya Opereshen ya Msako kwa Watuhumiwa wa wizi pamoja na Madumu ya Pombe haramu ya Gongo Lita 369 ambapo watu 15 wamekamatwa wakifanya Biashara ya Kuuza na Kusafirisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...