Kufuatia
Wimbi la Uvuvi haramu mkoani Kigoma
,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdalla Hamisi Ulega jana alishuhudia uchomwaji wa zana haramu za Uvuvi
katika kijiji cha Buhingu kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza,mkoani
Kigoma.
Mwenyekiti wa kikundi cha Usimamizi shirikishi rasilimali za Uvuvi (BMUs) katika Kijiji cha Buhingu Bw.Richard Nkayamba amemweleza naibu Waziri kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanakomesha Uvuvi haramu katika Kijiji cha Buhingu na kuweka mazingira safi.
"Kwa kiasi kikubwa tumedhibiti Uvuvi haramu pamoja na kutoa elimu kwa Jamii za Wavuvi, kuhusu Umuhimu wa Uvuvi endelevu kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi shirikishi BMUs 21 pamoja na shirika lisilokuwa la kiserikali la Tuungane lililopo katika kijiji cha Buhingu"alisema Nkayamba
Aliongeza,"Tunakamata nyavu haramu bila kujali ni za nani,na hii inatujengea chuki kwa wamiliki wa Nyavu husika"Akiongea na uongozi wa Halmashauri ya Uvinza pamoja na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo,Ulega amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Uvinza kuona ni namna gani wanaweza kuziwezesha BMUs zilizopo kijijini hapo.
"Naombeni sana mziwezeshe hizi BMUs wapeni tenda za kukusanya Maduhuri ya Samaki kwa Wavuvi hawa ili hizi BMUs ziweze kujiendesha zenyewe"Mhe.Ulega alisisitiza kuwa kama wakipewa BMUs kukusanya Maduhuri basi watakuwa wametengeneza ajira kwa Vijana hao.VileVile aliwaasa sana BMUs kuwa Waadilifu ili waweze kuaminiwa"
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishuhudia uteketezaji wa zana haramu za uvuvi katika Ziwa Tanganyika,kwenye mwambao wa kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali na wananchi wa kijiji cha Buhingu mkoani Kigoma.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akimkabidhi cheti ndugu Mapango Thomas cha utambuzi ili waweze kusimamia ipasavyo rasilimali za uvuvi

Mkuu wa Wilaya ya Uviza,Mwavua Mrindo akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali katika kijiji cha Buhingu mkoa wa Kigoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...