Na Robert Hokororo, Kishapu

Mvua kubwa ya upepo mkali imesababisha maafa katika vijiji vya Ukenyenge na Negezi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambapo imeezua paa za nyumba 37 pamoja na majengo Serikali.

Tukio hilo lilitokea saa 12 jioni ambapo majengo yaliyopatwa na maafa hayo ni ya pamoja na ofisi ya tarafa ya Negezi, ofisi ya afisa kilimo, ofisi ya TCRS.

Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Sahadrack Kengese alitembelea eneo hilo yalipotokea maafa akiwa amembatana na wataalamu kutoka halmashauri kwa ajili ya kufanya tathimini ya tukio hilo.Mratibu wa Maafa Wilaya, Ponsian Kuhabwa na Mwesiga Katunzi kutoka Idara ya Ujenzi waliungana na viongozi wa tarafa na kata na kufanya tathimini hiyo ambapo bado hasara iliyotokea haijafahamika.

Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa Tarafa, David Isanga mara baada ya tukio hilo uongozi wa tarafa na kata ulishirikiana na wananchi kuhakikisha wanawasaidia wenzao walioathirika ili kurudisha hali.Tathimini inaonesha kuwa hali ya maafa sio ya kutisha na ipo katika uwezo wa jamii kusaidiana na kuwa katika jengo la tarafa inaonyesha mahitaji mbalimbali ili kulirudisha katika matumizi.

Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa ni pamoja na ukarabati kufanyika haraka ili watumishi wapate sehemu za kufanyia kazi kwani sasa hivi wanabanana katika vyumba viwili vilivyosalimika.Aidha, timu ya tathmini ilishauri kuendelea kupanda miti mbele ya jengo hilo ili kupunguza kasi ya upepo na kutunza mazingira katika eneo hilo. Pia wananchi wameshauriwa kupanda miti na kujenga nyumba imara ambazo zitasitahimili mitikisiko ya matukio kama haya.
Picha mbalimbali zikionesha nyumba zilivyoezuliwa paa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha katika vijiji vya Ukenyenge na Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...