JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2017 amewasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali       na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasilisha fomu hiyo Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Sekretarieti        ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kazi inazofanya na amemtaka Kamishna      wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017.
“Mhe. Jaji Nsekela ikifika tarehe 31 Desemba, ambayo ni siku              ya mwisho kwa Mujibu wa Sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema” amesisistiza Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela amemshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo na amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma sio ombi.
“Viongozi hawaombwi kujaza fomu hizi, kuna baadhi wanadhani labda kutuletea hilo tamko ni fadhila, hapana, sheria ya nchi inahitaji hivyo   na kuna sababu zake za msingi” amesema Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela.
Aidha, Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuwasilisha taarifa ya akaunti yake ya benki sambamba na tamko hilo, na amekiri kuwa ameonesha mfano wa kuigwa na viongozi wengine.
Tamko la viongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni linatolewa kwa mujibu  wa kifungu cha 9 na cha 11 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Desemba, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma kwa ajili ya  kuwasilisha Fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kuwasili katika Makao makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma kwa Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katika Makao makuu ya ofisi hizo yaliyopo katika Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati akitoka katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya  Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi walio simama kando ya barabara inayopita mtaa wa Ohio wakati akitoka katika Ofisi za za Sekretarieti ya  Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...