Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia (kulia, akiwa na Makamu wake Michael Wambura) atakutana na Wahariri wa Habari za Michezo Jumatano Desemba 27, 2017.
Pamoja na mambo mengine Rais Karia atazungumzia miezi minne tokea uongozi uliopo umeingia madarakani pamoja na vitu vilivyofanyika katika muda huo.
Aidha Rais Karia ataelezea changamoto mbalimbali zilizopo TFF pamoja na njia gani inatumika/Itatumika kuweza kupiga hatua kwa mpira wa Tanzania.
Taarifa zaidi za mkutano huo wa Rais Karia na Wahariri,mahali utakapofanyika pamoja na mualiko utatolewa kwa vyombo vya habari.
Huu ni mkutano wa kwanza wa Rais Karia na Wahariri wa habari za Michezo tokea ameingia madarakani.
Rais Karia aliingia madarakani August 12, 2017 kwenye uchaguzi uliofanyika mkoani Dodoma baada ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi ambao pia uliwaingiza madarakani Michael Wambura kwenye nafasi ya makamu wa Rais. Wajumbe wa kamati ya utendaji waliongia madarakani kwenye uchaguzi huo ni pamoja na
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...