NA VICTOR MASANGU, MKURANGA
MAMLAKA ya mapato (TRA) Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani imefanikiwa kukamata tani 26 za mizigo ya aina mbali mbali ambayo ilikuwa imepakizwa katika malori mawili ya magari ikisafirishwa kinyemela kutokea kariakoo Jijini Dar es Salaam kuelekea mikoa ya kusini bila ya kuwa na risiti halali kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa TRA Wilaya ya Mkuranga Amosie Ernest alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa baada ya kuyakamata malori hayo walipoyapekuwa waliweza kubaini kuwa yamesheheni bidhaa nyingi ambazo hazijakatiwa risiti kwa mfumo wa mashine ya kielectroniki (EFD), hivyo walikuwa wanakwepa kulipa kodi.
“Ni kweli kwa sasa tupo katika msako mkali kwa ajili ya kuweza kugagua magari yote ambayo yanabeba miigo bila ya kuwa na risiti, na katika zoezi hili tumefanikiwa kuyakamata magari mawili makubwa ambayo yalikuwa yamebebeba mzigo ambao ulikuwa na bidhaa mbali mbali na baada ya kufanya uchunguzi tuliweza kuona kuwa kuna mapungufu makubwa kutokana na wahusika kutokuwa na risiti hivyo magari tumeyakamata yote,”alisema Ernest.
Pia alisema kwamba mizigo hiyo ambayo ilikuwa inasafirishwa kutokea maeneo ya kariakoo Jijijini Dar es Salaam kuelekea mikoa ya kusini ilikuwa na mapungufu makubwa kutokana na baadhi ya mizigo mingine ilikuwa haina risiti kabisa na baadhi ya mingine ilikuwa imekatiwa risiti kwa gharama ambayo ni ndogo ukilinganisha na bei iliyonunuliwa dukani.
Kwa upande wake Afisa elimu na huduma kwa mlipa kodi wa TRA Mkoa wa Pwani Kapera Bakari amebainisha kuwa thamani ya awali ambayo wameifanya wamebaini mizigo hiyo ambayo ina jumla ya thamani ya shilingi milioni 84 imekwepa kulipiwa kodi kihalali ni zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 16 ambazo zilitakiwa kuingia serikalini.
Aidha Kapera alibainisha kuwa serikali ya awamu ya tano kwa sasa ipo macho katika kuhakikisha inakusanya mapato yake hivyo amewaasa wafanyabiashara wote Mkoa wa pwani kuachana na tabia ya kununua mizigo dukani bila ya kuwa na risiti ya aina yoyote kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kupoteza mapato kutokana na tabia ya ukwepaji wa kulipa kodi kwa kutumia mashine za EFD.
Mmoja wa madereva ambaye amekamatwa kutokana na kuhusika na tukio hilo ajulikanaye kwa jina la Hamis Abibu amesema kwamba mizigo ambayo alikuwa ameipakia katika gari yake akutambua lolote kama imenunuliwa bila ya kuwa na risiti ambazo zinastahili.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Sevelini Lalika ambaye nae alifika katika eneo la tukio ameipongeza TRA kwa juhudi wanazozifanya za kumuunga Rais wa awamu ya tano Dk,John Pombe Mgaufuli katika kuhakikisha wanakusanya kodi ipasavyo na kuwabana wale wote wenye tabia ya kukwepa kulipa kodi ya serikali kwa makusudi.
MALORI hayo mawili ya magari ambayo yamekamatwa na TRA yamekutwa yamesheheni bidha mbali mbali zikiwemo mikeka, viatu, mashuka, baiskeli,sabuni, spea mbali mbali za pikipiki, zimeingiza hasara ya zaidi ya kisi cha shiingi milini 16 kutokana na kukwepa kulipa kodi kihalali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...