Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

Uamuzi kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inayo mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi Ama la, dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano  kutolewa kesho.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa baada ya kumaliza kusikiliza hoja za upande wa jamhuri kufuatia mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi.

Wakili wa Serikali Shadrack Kimaro alidai kuwa hoja ya Mawakili wa utetezi kuwa mahakama ya Kisutu inamamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo kwa sababu ipo chini ya Sh 1 bilioni  siyo sahihi.

Amedai, ni dhahili kuwa makosa wanayoshtakiwa nayo washtakiwa ni ya uhujumu uchumi na mahakama pekee yenye mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo ni Mahakama Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu mahakama ya Mafisadi.

Ameongeza, mahakama za chini kama Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo labda kuwepo na kibali kutoka kwa DPP kitakachoipa mahakama ya chini cha kulipa mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo.

Kufuatia hoja hiyo, Hakimu Kimaro aliiomba mahakama kutupilia mbali hoja za upande wa utetezi na kwamba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Wakili wa utetezi, Denis Msafiri akijibu hoja hiyo alidai, marekebisho ya sheria ya uhujumu uchumi ya 2016 yanaipa mahakama ya Kisutu mamlaka ya  moja kwa moja kuisikiliza kesi hiyo.

"Kosa lolote lililopo chini ya Sh 1 bilioni haliwezi kusikilizwa na Mahakama Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi ni Mahakama za chini ikiwamo Mahakama ya Kisutu". Amedai msafiri.

Aidha amedai, kibali cha DPP cha kuipa mamlaka mahakama kusikiliza kesi kilipaswa kupelekwe mahakamani hapo pamoja na hati ya mashtaka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Kesho kwa mahakama kutoa maamuzi, pia ameamuru washtakiwa wapelekwe polisi.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Pius Hilla aliomba washtakiwa wapelekwe magereza kwa sababu kuendelea kuwa mikononi mwa polisi kuna suala la gharama na polisi hawana fungu hilo pia watuhumiwa ambao wameishasomewa mashtaka hawaruhusiwi kukaa polisi zaidi ya siku Tatu.

 Wakili Nehemia NNkoko aliomba mahakama kusimamia amri yake kama ilivyoitoa na kuomba mahakama iendelee na oda yake ilivyoitoa jana.

Hakimu Nongwa alisema suala la gharama haliwezi kukwepeka pale Haki inapotafutwa na kuamuru washtakiwa wapelekwe polisi hadi Leo atakapotoa uamuzi kama mahakama hiyo ina mamlaka ama la.

Madabida na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita  ya uhujumu uchumi ikiwamo kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi ' ARV’s ' na kusababisha hasara ya Sh 148 milioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...