Na: Frank Shija - MAELEZO
Serikali
kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezifutia leseni za uendeshaji wa
shughuli za kibenki Benki tano ambazo zimeshindwa kukidhi matakwa ya
sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
Akizungumza kuhusu hatua hiyo Gavana wa Benki Kuu anayemaliza muda wake amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa kufuatia benki hizo kushindwa kutekeleza matakwa ya kisheria yaliyozitaka benki zote za kijamii kuongeza kiwango hicho cha mtaji ili ziweze kujiimarisha licha ya kupewa muda wa kipindi cha miaka mitano ulifikiwa tamati tarehe 31 Juni 2017.
“Maamuzi haya tunayafanya baada ya Benki zote nchini kupewa muda wa miaka mitano na nusu yakuweza kukidhi matakwa ya sheria, lakini mpaka ilipofika tarehe 31 Desemba 2017 jumla ya benki Nane zilishindwa kuongeza mtaji uliohitajika kati ya hizo Benki Tano zilishindwa kuwasilisha mpango kazi wa kuonyesha namna zitakavyo kuwa endelevu,” alisema Profesa Ndulu.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anayemaliza muda wake Profesa Beno Ndulu akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu kuzifutia leseni ya uendeshaji wa shughuli za kibenki baadhi ya benki hapa nchini katika mkutano uliofanyika BoT Jijini Dar es Salaam leo. Takribani benki tano zimefutiwa leseni zao na nyingine tatu zimeongezewa muda ili kukidhi vigezo. Katikati ni Gavana Mteule wa BoT Profesa. Florens Luoga na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Amana Richard Malisa.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano baina yao na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzani (BoT) anayemaliza muda wake Profesa Beno Ndulu akiwa ameambatana na Gavana mteule wa Benki hiyo Profesa Florens Luoga leo jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anayemaliza muda wake Profesa Beno Ndulu akipeana mkono wa kwaheri na Gavana mteule wa Benki hiyo Profesa Florens Luoga. (Picha na Frank Shija – MAELEZO)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...