Na Mwandishi Wetu
Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imenunua vitendea kazi vipya na
vya kisasa kwa ajili ya bandari ya Mtwara ili kuongeza ufanisi.
Vifaa
hivyo ambavyo tayari baadhi vimeshawasili bandarini hapo ni pamoja na
mzani wa kisasa ‘Movable Weigh Bridge’ wenye uwezo wa kupima hadi tani
100 ambao tayari unatumika.
Vifaa
vingine vilivyonunuliwa na vinavyotarajiwa kuwasili kuanzia mwezi
Januari, 2018 ni pamoja na ‘Reach Stalker’ mbili mpya zenye uwezo wa
kubeba tani 40 kwa wakati mmoja.
Mkurugenzi
Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko ameyasema hayo wakati wa
majumuisho ya ziara za Kamati za Bodi za Wakurugenzi wa TPA
zinazoshughulikia TEHAMA na Utelekezaji na ile ya Uwekezaji na Maendeleo
ya Biashara.
Wakurugenzi
wa Bodi za Kamati hizo ambazo ziliongozwa na Mwenyekiti, Dkt. Jabiri K.
Bakari, ni pamoja na Jayne K. Nyimbo, Renatus Mkinga, Aziz M. Kilonge
na Jaffer S. Machano.
Kamati
hizo zilitembelea miradi mbalimbali iliyopo Bandari za Mtwara na Lindi
na kutoa maelekezo kadhaa ambayo ni muhimu katika kuendeleza bandari
hizo ili kuongeza huduma zake.
Akizungumzia
vifaa vipya vilivyowasili na vinavyotarajiwa kuwasili hivi karibuni,
Mhandisi Kakoko amesema ununuzi wa vifaa hivyo ni utekelezaji wa mipango
ya kuifanya bandari hiyo kuwa ya kisasa zaidi.
“Ununuzi
wa vifaa tunaofanya sasahivi utasaidia kuboresha na kuimarisha zaidi
utendaji kazi wa bandari ya Mtwara na kuongeza ufanisi zaidi,” amesema
Mhandisi Kakoko.
Mkuu wa bandari ya Mtwara, Nelson Mlali (Kulia) akitoa maelezo kwa Wakurugenzi wa Bodi wa TPA wa Kamati za TEHAMA na Utekelezaji pamoja na ya Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara mara baada ya wajumbe wa kamati hizo kufanya ziara ya kikazi banddari ya Mtwara hivi karibuni.
Mkuu wa bandari ya Mtwara, Nelson Mlali (Kulia) akitoa maelezo kwa Wakurugenzi wa Bodi wa TPA wa Kamati za TEHAMA na Utekelezaji pamoja na ya Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara mara baada ya wajumbe wa kamati hizo kufanya ziara ya kikazi banddari ya Mtwara hivi karibuni.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...