Klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club imetwaa ubingwa wa Tanzania wa waogeleaji chipukizi wenye umri kati ya miaka saba na 14 kwa mara ya pili mfululizo baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 3,144.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya timu sita, yalimalizika Jumamosi jioni kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Haven of Peace Academy (Hopac) jijini.
Haikuwa kazi rahisi kwa Dar Swim Club kutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo kutokana na ushindani mkubwa kutoka kwa klabu za Taliss na Bluefins ambao zilionyesha upinzani wa hali ya juu.
Taliss ilimaliza katika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 2,966 huku Bluefins ikimaliza ya tatu kwa kupata pointi 2,945 na Champion Rise ikishika nafasi ya nne kwa kupata pointi 329.
Nafasi ya tano ilichukuliwa na timu ya Wahoo ya Zanzibar kwa kupata pointi 222 na klabu ya Mwanza International School ikimaliza ya sita kwa kupata pointi 44 katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kituo cha ITV, Coca Cola, Print Galore, Label Promotions, Kisima Water, IST, JNC Events Support &co limited, Kalu Photography na Knight Support.
Waogeaji wa kike wa klabu ya Dar Swim Club ndiyo waliochangia ushindi kwa kiasi kikubwa katika mashindao hayo baada ya kuwa wa kwanza kwa kujikusanyia pointi 1,706 na kufuatiwa na Taliss waliopata pointi 1,480 na Bluefins kwa kupata pointi 1,000.
Wahoo walishika nafasi ya nne kwa upande wa wasichana kupata pointi 190 na kufuatiwa na Mwanza (44) na Champions Rise katika nafasi ya sita kwa kupata pointi 30.
Kwa upande wa wavulana, klabu ya Bluefins ilishika nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 1,755 na kufuatiwa na Taliss (1,321) na Dar Swim Club (1,243), Champion Rise ( 329) na Wahoo katika nafasi ya tano kwa kupata pointi 32.
Katibu Mkuu wa DSC, Inviolata Itatiro aliwapongeza wachezaji na makocha wa klabu hiyo kwa kufanya vyema katika mashindano hayo na kuendelea kuwa mabingwa.
Inviolata alisema kuwa kujituma kwa wachezaji, makocha, viongozi na wazazi kumeiletea sifa timu hiyo.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya waogeleaji chipukizi 182 ambao walishindana katika mita 50, 100 na 200 katika staili tano butterfly, freestyle, breaststroke, backstroke na Individual Medley (IM).
Wachezaji wa klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club wakifurahia ubingwa wa Tanzania wa waogeleaji chipukizi wenye umri kati ya miaka saba na 14
Wachezaji wa klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club wakifurahia kombe la ubingwa wa Tanzania wa waogeleaji chipukizi wenye umri kati ya miaka saba na 14
Wachezaji wa klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club wakipozi na kombe la ubingwa wa Tanzania wa waogeleaji chipukizi wenye umri kati ya miaka saba na 14
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...