Usimamizi
mzuri na utekelezaji wa Sera mbalimbali za kuwawezesha wananchi
kushiriki kikamilifu kujenga na kumiliki uchumi, kumeifanya Tanzania
kuibuka kinara miongoni mwa nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara
kwa kuwa na Uchumi Jumuishi (Inclusive Economy) unaokua duniani.
Taarifa iliyotolewa na Word Economic Forum kupitia mradi wake wa ‘The Inclusive Development Index’, imeitaja Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na ya 48 kati ya nchi 103 zilizofanyiwa tathmini ya nchi zenye Uchumi Jumuishi duniani,
Katika orodha ya kumi bora, nchi zilizofuatia na nafasi ziliyoshika kidunia ni pamoja na Ghana (52), Cameron (53), Burundi (55), Namibia (56), Rwanda (57), Uganda (59), Mali (60), Senegal (61) na Nigeria (63).
Takwimu za ukuaji huu zinaakisi moja kwa moja kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akielezea kutaka uchumi wa Tanzania umilikiwe na wananchi kwa njia mbalimbali ikiwemo kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda ambapo watanzania wengi hivi sasa wamekuwa wakitekeleza sera hiyo kwa kuanzisha viwanda vikubwa na vidogo.
Mtaalamu Mbobevu wa masuala ya Uchumi na Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi ameeleza kuwa takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo zinatafsiri kuwa uchumi wa Tanzania unaelekea kumilikiwa na watu wengi zaidi jambo ambalo litasaidia kupunguza pengo la kipato kati ya walionacho na wasionacho.
Profesa Ngowi ameeleza kuwa uchumi wa aina hiyo unawashirikisha wananchi kumiliki uchumi na kuwafanya watu wengi kufaidi matunda ya ukuaji wa uchumi wa nchi.
“Taarifa hizi ni njema kwani kitaalam tunaita broad based economy ambapo watu wengi wanashirikishwa kumiliki uchumi na wengi wanafaidi,” alieleza Profesa Ngowi na kuongeza kuwa kuna nchi zingine zinauchumi mzuri lakini unamilikiwa na watu wachache na kufanya kuwa na pengo kubwa kati ya walionacho na wasionacho.
Katika siku za hivi karibuni, Taasisi mbalimbali duniani zimekuwa zikitoa ripoti zikiielezea Tanzania kupaa kiuchumi ambapo ripoti za Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Taasisi ya Goldman Sachs ya Marekani hivi karibuni zilitabiri kuwa wakati uchumi wa dunia utakua kwa wastani wa asilimia 3.0 hadi 4.0, ukuaji wa uchumi wa Tanzania unatajwa kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika ukitarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 katika mwaka 2018.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...