SHULE ya  Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam imeng’ara kwenye matokeo ya darasa la nne kwa kufanikiwa kuwa ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam na kutoa wanafunzi saba kati ya 10 walioingia kumi  bora kitaifa.

Katika matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), shule hiyo pia imefanikiwa kutoa wanafunzi wa kike saba bora kitaifa miongoni mwa wasichana 10 walioingia kumi bora kitaifa na mwanafunzi bora kitaifa.

Wanafunzi waliofanikiwa kuingia 10 bora kitaifa ni Rahma Khatibu (Hazina), Fildaus Abbas (Hazina),  Martha Shayo (Hazina), Momy Lawrence (Hazina), Zayyana   Nassoro (Hazina), Kokudyness Rweyemamu (Full Gospel), Jesca Nenula (Hazina), Lailaty Nurdin (Hazina), Sharp Gabukambwe (Mungu Bariki) na Muhamed Hoti (Mudio Islamic).

Wasichana walioingia 10 bora kitaifa ni Rahma Khassan (Hazina), Fildaus Msafiri (Hazina), Martha Shayo (Hazina), Momy Laurence (Hazina), Zayyana Nassoro (Hazina), Kokudyness Rweyemamu (Full Goaspel), Jesca Nenula (Hazina), Lailaty Balii (Hazina), Sala Elias (Mwilamvya), Veneranda Richard (Mwilamvya).

Akizungumza, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Patrick Cheche, alisema kwenye kundi la wanafunzi chini ya 40 shule ya Hazina imekuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema shule hiyo imefanikiwa pia kuwa ya tatu kitaifa na ya kwanza kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa miaka zaidi ya 10 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo wamekuwa wakipata mafanikio makubwa mwaka hadi mwaka kwenye matokeo ya kitaifa.

Alitoa mfano kuwa shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kitaaluma kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na hadi Taifa na kumekuwa na mabadiliko chanya.

Cheche alisema malengo yao ni kuendelea kufundisha kwa bidii sana ili kuendelea kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa na kusaidia watoto wengi wa Tanzania kupata elimu bora.
 Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Hazina, Patrick Cheche akimpa zawadi mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la nne, Rahma Khatibu. Wengine wanaofuata ni Fildaus Abbas, Lailaty Nurdin, Jesca Nenula na Zayyana Nassoro ambao wote wameingia kumi bora kitaifa kwenye matokeo hayo.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam wakishangilia baada ya shule yao kuibuka ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam kwenye matokeo ya darasa la nne na kuwa ya   tatu kitaifa yaliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) pamoja na kutoa mwanafunzi bora kitaifa Rahma Khatibu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...