Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe akiwapongeza wajumbe wa
kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo kwa ubunifu waliyofanya katika siku
ya uzinduzi uliyofanywa hivi karibuni na Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, katika Kikao cha Tathimini ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Leah Kihimbi ambaye ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Sanaa kutoka Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na
kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi.Shani Kitogo ambaye ni Mkurugenzi
Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bi.Leah Kihimbi (kulia) ambaye ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Sanaa kutoka Wizara Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo akieleza mafanikio ya uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) ikiwemo
kupokea maombi kutoka taasisi mbalimbali kuomba wanakamati kwenda kutoa mafunzo
kuhusu suala la uzalendo kwa watumishi wa ofisi zao,katika kikao cha tathimini
ya uzinduzi wa Kampeni hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya
Uzalendo Bi.Joyce Fissoo ambaye ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini
akitoa mapendekezo katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa Kampeni ya
Uzalendo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuhusu Makala ya
viongozi na wadau waliyozungumzia suala la uzalendo kwa taifa itakapo kamilika
iweze kusambazwa nchini nzima katika Shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya kuwapa
fursa watoto hao kujifunza kuhusu uzalendo.
Mjumbe wa Kamati ya
Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bw.Mrisho Mpoto akitoa maoni ya mambo
mbalimbali yanayoweza kufanikisha kampeni hiyo kuwa endelevu ikiwemo wajumbe
kufanya tafiti kwa nchi zenye uzalendo kama China kwa lengo la kuhakikisha
taifa linaelewa umuhimu wa uzalendo na manufaa yake katika kikao cha tathimini
ya uzinduzi wa kampeni hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...