Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ilikuwa ni heshima kubwa ugenini wakati Rais wetu (mstaafu) Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa digrii ya heshima ya uzamili ya Chuo Kikuu cha Newcastle, Australia, siku ya Alhamisi, Julai 30, 2015.

    Sherehe hiyo ilifunguliwa kwa wimbo mkongwe wa Kiswahili uliotukuka sana ukiisifu nchi yetu (moja na pendwa) ya Tanzania, “TANZANIA, NAKUPENDA KWA MOYO WOTE.”

    Kwenye sherehe hiyo, wimbo huo uliimbwa kwa Kiswahili (kwa umahiri mkubwa) na mmoja wa wenyeji wa Australia, Bibi Bernadette Mathias, akisindikizwa na mpigapiano mwanaume.

    Hapo juu, nakala ya wimbo huo wa Bernadette Mathias ndio inabariki video ya ufunguzi wa (na hitimisho la) MAKALA YA RAIS, na kutayarishwa na wafanyakazi wake wanaojirozesha mwishoni (bila kutambua kwa kutaja mwimbaji wa nakala ya wimbo huo), kama ilivyo hapo juu.

    Ugenini, ni safi sana kusikia wenyeji wetu wakiimba nyimbo zetu kutusifia; tunajiona tu nyumbani. Lakini haiingii sana akilini hata kidogo kutosikia sauti ya nakala ya wimbo wa “TANZANIA, NAKUPENDA KWA MOYO WOTE” iliyoimbwa na baadhi ya wasanii wazalendo Watanzania (wakiwemo polisi na jeshi la ulinzi) waliowahi kuimba wimbo huo?

    Kwa nini sauti ya Mwaustralia izamishe sauti nzuri za wasanii hao wetu? Ninapendekeza tuachane na hiyo nakala ya Waustralia na kuweka nakala kutoka maktabani hapo Ikulu, Maelezo au Radio Tanzania ya wasanii wetu hao ili ipambe mwanzo na mwisho wa hiyo MAKALA YA RAIS.

    ReplyDelete
  2. Kuniradhini:

    Hapo juu nimemtaja Bibi Bernadette Mathias, jina nililokopi kutoka mitandao ya jamii ya nyumbani. Jina hilo la pili ni kosa. Jina lake sahihi ni Bernadette Matthias (ambaye ni mwalimu wa sauti na mwanakwaya wa Chuo Kikuu cha Newcastle, Australia.)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...