Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amezitaka Halmashauri na Manispaa zote nchini kuzipa kazi  ya kukusanya ushuru wa samaki na mazao yatokanayo na samaki BMUs ili ziweze kujiendesha na kusimamia ipasavyo Rasilimali za Uvuvi.

Ulega ameyasema hayo katika Mkutano wa kuzungumza na Jamii ya wavuvi  Kilwa - Kivinje. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa ameahidi kuzipa kazi  hiyo ifikapo Mwezi Machi, 2018 baada  ya kukamilisha zoezi la  Upitishaji wa Kanuni ndogondogo kwa kila BMUs ambapo kwa wilaya ya Kilwa zipo sita (6).

Aidha, Mhe. Ulega amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa kuhakikisha kuwa Mtambo wa Kuzalisha barafu katika mwalo wa Kilwa - Masoko unafanya kazi  ndani ya siku 14.

Akijibu maswali na hoja za wananchi huku akishangiliwa, Mhe. Ulega, amewaahidi wananchi  katika Wilaya hiyo kurudi mwezi Machi kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.

Katika kuhitimisha ziara yake  Mhe. Ulega ameshiriki zoezi la  Upigaji Chapa Mifugo katika kijiji cha Mpara, eneo la  magereza ambapo kwa siku ya leo  tu tarehe 10/01/2018 Jumla ya Ng'ombe 198 wamepigwa Chapa. Jumla ya ng'ombe  40,000 wanatarajiwa kupigwa Chapa katika wilaya ya Kilwa.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi katika soko kuu la samaki la mkoa wa Lindi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na watendaji mbalimbali, wavuvi ambapo amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa kuhakikisha kuwa Mtambo  wa Kuzalisha barafu katika mwalo  wa Kilwa - Masoko unafanya kazi  ndani ya siku 14. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwaelekeza  namna bora ya kupiga chapa mifungo ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishiriki zowezi la upigaji cha mifungo kijiji cha Mpara mkoa wa Lindi.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Zabron Bugingo(katikati) akishiriki zowezi la upiji chapa mifungo, kushoto ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishuhudia zowezi hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kilwa,Zabron Bugingo (wakwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega kuhusu mkakati wa Halmashauri wa  kuongeza uzalishaji wa Mikorosho katika kituo cha Mpara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...