Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha wa USD 300,000 ameshindwa kufika katika Mahakamani kwa sababu ana matatizo ya figo.
Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika lakini amepewa taarifa kuwa Aveva anaumwa.
Mbali ya Aveva mshtakiwa mwingine ni katibu wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' ambapo Swai ameeleza kuwa amepewa taarifa kutoka Magereza kuwa Aveva hakufika mahakamani kwa sababu ana matatizo ya figo.
Aliongeza kudai kuwa bado hawajapatiwa nyaraka walizoziomba kutoka ofisi ya Aveva na pia aliiomba mahakama iwaruhusu wakamuhoji mshtakiwa Kaburu.
Baada ya hayo, Hakimu Nongwa alikubaliana na maombi ya kutaka kumuhoji mshtakiw kaburu na kuwataka wafuate utaratibu. kesi hiyo imeahirishwa hadi January 25,2018.
Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...