Na Yasin Silayo

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limeandaa mfumo wa taarifa za kijiografia za wateja, maarufu kwa jina la GIS, kwa lengo la uboreshaji wa huduma za usambazaji umeme, ambapo sambamba na ujio wa mfumo huo TANESCO iliandaa  mafunzo maalumu kwa wafanyakazi wa Shirika hilo kwa Kanda ya Dar na Pwani iliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani. Hayo yamebainishwa na Naibu Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO Anayesimamia masuala ya Usambazaji umeme na huduma kwa wateja Bi. Joyce J Ngahyoma (pichani, aliyesimama).
Akiongea katika kikao cha tamati ya mafuno hayo Bi. Joyce alisema kuwa Mfumo huo wa uboreshaji wa huduma za usambazaji umeme (GIS) kanda ya Dar na Pwani ulibuniwa na TANESCO kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usambazaji umeme kwa kupitia mjumuisho wa pamoja wa taarifa zote za wateja, miundombinu ya kusambaza umeme pamoja na ramani ya mifumo ya umeme yenye taarifa za wateja wote kulingana na taarifa za kijografia za maeneo yao waliyoko.
Aliongeza kuwa TANESCO Iliamua kuja na mfumo huu kama suluhisho kutokana na Kanda ya Dar es salaam na Pwani, kuwa na changamoto nyingi za kihuduma zinazotokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya umeme kila uchwao. Ongezeko hili la mahitaji ni kutokana na ujenzi wa majengo marefu ya kibiashara pamoja na viwanda vya uzalishaji mali katika maeneo mbalimbali ya katikati ya Jiji na Mkoa wa pwani, hasa Kariakoo, Ilala, Kinondoni, Kigamboni na maeneo ya kiviwanda yaliyopo na yale mapya yanayoanzishwa katika Kanda ya Dar wa Pwani.

Aidha Bi. Ngahyoma alibainisha kuwa ni matumaini ya Uongozi wa Shirika na Serikali kwa ujumla, kuwa mafunzo hayo yanayoambatana na matumizi ya mfumo wa taarifa za kijiografia (GIS) yatasaidia Shirika kuimarisha huduma maradufu hivyo kuchochea zaidi ukuwaji wa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Baada ya kukamilika kwa mfumo huu wa GIS Katika kanda ya Dar na Pwani, lengo la TANESCO ni kupanua zaidi mfumo huu katika Mikoa mingine.
Kutokana na mafunzo yaliyotolewa katika semina hiyo na matumizi ya mfumo wa GIS, yatarahisisha na Kuboresha huduma kwa wateja na kuongeza ufanisi wenye tija katika huduma zaShirika. Maboresho yatakayojumuisha kuwafikia wateja kwa wakati na haraka zaidi yanapotokea matukio ya dharura, udhibiti wa wizi wa umeme, ukusanyaji haraka mapato ya Shirika, kuchukua vipimo vya wateja wapya wanaohitaji kuunganishwa umeme (Service line Survey) kwa haraka kupitia mfumo huu kutokea ofisini, kuimarisha usimamizi mzuri wa miundombinu ya usambazaji umeme kwa wateja huko mitaani pamoja na kurahisisha ukaguzi wa taarifa za mauzo ya Shirika na kulinda Transfoma za usambazaiji umeme zisiungue ambapo ilielezwa kuwa Shirika linatarajia mageuzi makubwa ya kihuduma kwa wateja kupitia mfumo huo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Wa TANESCO anayesimamia masuala ya Usambazaji Umeme na Huduma kwa Wateja Bi. Joyce Ngahyoma, akiongea na wafanyakazi wa TANESCO walioshiriki mafunzo ya mfumo huo mpya Wa GIS yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za TANESCO Mkoani wa Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...