Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema suala la maji Mkuranga ni tatizo la muda lakini sasa matumaini yameanza kuonekana baada ya benki ya Dunia kuleta mradi wa maji wa visima 29 utakaokuwa na thamani ya zaidi ya bilioni mbili.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwanambaya, amesema kuwa mradi wa maji utakuwa historia kutokana na hatua zinazochukuliwa na serikali. Amesema katika ziara zake amekuwa akikutana na changamoto za maji lakini hatua zimeanza kuchukuliwa kwa kiangazi cha mwaka huu maji yatakuwa tayari.
Katika Mkutano huyo amehidi kutoa bati 100 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili ya shule ya Msingi Mwanambaya.
Naibu Waziri huyo ameiomba kamati ya kijiji kukutana na mganga Mkuu ili waweze kuipandisha dispensari hiyo kwenda kituo cha afya.
Mbali na hilo wananchi wa kijiji cha Mwanambaya wamemuomba mbunge Ulega kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kulipwa stahiki zao za kupitiwa na mradi wa mabomba ya gesi ya Kilwa Energy.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...