Watoto wenye saratani ambao wanamekuwa wakihudumiwa na Kituo cha Tumaini la Maisha kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)wamepatiwa msaada wa fedha kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali ikiwamo na lishe bora.
Kampuni ya Simu ya Vodacom leo imetoa msaada wa Sh. 30 milioni kwa kituo cha ikiwa ni jitihada za kuiunga serikali mkono katika mipango yake za kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa kundi hilo.
Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru ameishukuru kampuni hiyo simu kwa kuwasaidia watoto hao na ameiomba iendelee kuwaisaidia watoto hao ili kuwajengea uwezo wa kuwa na afya bora.
“Napenda kutoa shukrani kwa Vodacom kwa miaka kadhaa kuendelea kusaidia Tuamaini la Maisha,” amesema Profesa Museru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akipokea mfano wa hundi ya Shilingi 30 milioni ambazo zimetolewa na Kampuni ya Simu ya Vodacom kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye saratani. Kutoka kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Mawasilino wa Kampuni ya Vodacom, Jackline Materu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la Maisha, Dkt. Trish Scanlan na Zuhura Mawona ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Uuguzi Muhimbili.
Watoto wenye saratani wakifurahia jambo kabla ya kupatiwa msaada wa Shilingi 30 milioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...