Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt.Henry Mambo (wa pili kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt.(Mstaafu) George Mkuchika (wa tatu kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kukitembelea chuo hicho tawi la Singida mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Chuo cha utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Singida, Sijali Kolojelo akisoma risala ya mafanikio na changamoto za TPSC tawi la Singida wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) George Mkuchika (katikati) alipotembelea TPSC tawi la Singida mwishoni mwa wiki kushoto kwa Waziri wa ni Mkuu wa TPSC Dkt. Henry Mambo.
Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt.Henry Mambo aliyesimama akisoma risala fupi ya makaribisho kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt.(Mstaafu) George Mkuchika aliyekaa mara baada ya kuwasili TPSC tawi la Singida mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya watumishi wa TPSC tawi la Singida na wageni wengine wakimsiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt.(Mstaafu) George Mkuchika (hayupo pichani) mara baada ya kuwasili TPSC tawi la Singida mwishoni mwa wiki.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...