*Asisitiza kahawa iuzwe kwa mfumo wa ushirika
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa wilaya ya Songea mkoani
Ruvuma wajikite kwenye zao la kahawa ili wawe na zao mbadala la
biashara.
Ametoa
wito huo leo (Ijumaa, Januari 5, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa
kijiji cha Lipokela na vijiji jirani, wilayani Songea mara baada ya
kukagua shamba la kahawa la Aviv Tanzania lenye ukubwa wa hekta 1,990.
“Limeni
kahawa ili mpate fedha sababu zao hili ni la biashara. Kahawa ni
miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo Serikali ya awamu ya tano
imeamua kuyawekea mkazo ili yaweze kuongeza tija kwa wakulima na kuinua
uchumi wa Taifa”.
“Tumeamua
kuweka mkazo kwenye mazao matano ya pamba, kahawa, chai, korosho na
tumbaku kwa sababu yanaleta tija na kuliingizia Taifa fedha za kigeni,”
alisema na kuongeza:
“Tumefanya
tathmini na tumegundua udhaifu mkubwa mkubwa katika usimamizi wa mazao
haya ndani ya Serikali kuanzia ngazi ya Halmashauri.”
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi miche ya Kahawa, Mkulima wa zao hilo,
Remigius Njovu,i nayotolewa bure na Kampuni ya Molam Tanzania Limited,
kwa wakulima wa zao la Kahawa, baada ya kukagua kitalu cha miche ya
kahawa katika Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha
Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani
Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Molam
Tanzania Limited, Medappa Mg, wakati akikagua kitalu cha miche ya Kahawa katika
Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea,
Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma
kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Molam Tanzania Limited, Medappa Mg, wakati alipotembelea Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa ufafanuzi wa miche ya Kahawa, na mkulima wa zao hilo wakati akikagua kitalu cha miche ya kahawa katika Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...